Njia tatu (3) za kumnasa msomaji asome kitabu chako
Kitabu kinaandikwa ili kisomwe lakini si rahisi kumnasa msomaji akasoma kitabu chako bila kukiacha hata akakimaliza. Unavyokianza kitabu chako ndiyo jambo muhimu zaidi kwa sababu hakuna msomaji atasoma sentensi inayofuata, kisha inayofuata na inayofuata kama sentensi ya kwanza haikumfanya kuvutika kusoma zaidi.
Ishara tatu kwamba wasomaji hawamalizi kusoma kitabu chako
Si kila msomaji anayenunua kitabu atakisoma, wengine wanasoma kidogo tu, na wengine hawasomi kabisa. Lakini si waandishi wengi hufahamu jambo hili, furaha yao huwa “nimeuza kitabu, nimeingiza hela”. Kwenye tasnia ya uandishi, kuingiza pesa pekee si lengo la mwisho, kuona kwamba wasomaji wameelemika na wameburudika baada ya kusoma kitabu chako si jambo la kupuuzwa wala kupungunguzwa uzito wake.
[New book release] The Epic Novel, 'Yes, I Did It' is now available.
The epic novel – Yes, I Did It – that you have been waiting for is out. The novel is a sequel to It can't be TRUE. The main character is the same Albert Mukasa - the infamous Ugandan spy. The novel tackles the issue of children sacrifice in Uganda and the powers/ forces behind the heinous crime. There are enough intrigues, twists and turns to make you spellbound from the beginning to the end. If you enjoyed the It can't be TRUE, you will certainly love this more.
Kuwa mwandishi serious inataka nini?
Msomaji anaposoma kitabu cha mwandishi fulani huwa anakutana na mambo ambayo yatampa picha ya kumuona mwandishi yupo serious au la. Kwa bahati mbaya, wasomaji wengi wanapomwona mwandishi hayupo serious hubaki na dukuduku moyoni bila kumpa mwandishi mrejesho wa kitabu chake. Hii sio poa hata kidogo lakini ndio uhalisia wa mambo ulivyo
Jinsi ya kusoma kitabu ukiwa mtandaoni
Zamani kidogo ilikuwa huwezi kusoma kitabu kwa kutumia simu janja yako, tabuleti au kompyuta yako. Kusoma kitabu ingekutaka uwe na nakala ngumu, utulie mahali usome au uende maktaba iliyo jirani na wewe ili usome kitabu. Kama ungekuwa safarini, mfano kwenye daladala, ingekupasa utembee na nakala yako ili usome, sasa fikiria mtu aliyetaka kusoma vitabu vitano, si angebeba vyote atembee navyo? Shida gani hii!.
Badilisha maisha yako kwa kusoma kozi hizi nane (8)
Katika maswali haya, ni swali lipi linakuelezea wewe na umekuwa ukijiuliza bila majibu yake, na sasa ungetaka kuchukua hatua ya kufanyia kazi?; Je mimi nataka kujua jinsi ya kuandika kitabu? Je mimi nataka kujua jinsi ya kuuza kitabu changu zaidi? Je mimi nataka kutoa kitabu changu ila sijui nianzie wapi? Au Je mimi nataka kuwa bora zaidi kwenye uandishi wa vitabu?. Majibu yamepatikana, nakupa njia rahisi ya kutusua.
[New Book] Feedback: Underrated, Misused Leadership tool is now available.
The long wait is over, the new book Feedback: Underrated, Misused Leadership tool from Daniel Zake is now available. Daniel Zake is a seasonal Banker, working with a reputable financial institution for 12 years in leadership.
Mtazamo sahihi uletao mafanikio - Kitabu kipya kutoka kwa Ruth Heslone
Ingizo jipya la kitabu kwenye shelfu za vitabu ni kitabu cha MTAZAMO SAHIHI ULETAO MAFANIKIO ambacho kimeandikwa na Mwl. Ruth Heslone. Kitabu hiki ni moja ya projekti kubwa ambayo tumeifanya ndani ya mwezi wa kumi (10), tukihusika na kuhariri wake, kusanifu jalada na mpangilio wa ndani wa kitabu. Ni kazi bora sana ambayo tumeifanya.
[Hadithi fupi] Alisema nataka lakini...
Kama siku mbili tatu zilizopita kuna mzee mmoja hapa jirani na kwangu alimwona kijana mmoja anatembea huku macho kodo kwenye simu yake
Mzee akahamaki
"hawa vijana na siku hizi hovyo kabisa, badala atembee anaangalia
mbele yeye yuko busy na simu"
[Kozi] Hatua nne katika uandishi wa vitabu
Unazifahamu hatua nne (4) katika uandishi wa vitabu?. Watu wengi hufikia hatua ya kwanza, wengine hatua ya pili na ya tatu, na wachache sana huifikia hatua ya nne. Kuhusu hatua hizi nne (4), fahamu kwamba hatua zote nne zina uzito sawa, halafu zinategemeana, na zinaenda kwa mtiririko kwa kupandiana. Mwandishi hawezi kwenda hatua ya pili, bila ya kupitia hatua ya kwanza.
Naandikaje kitabu? sasa kimetoka!
Kitabu changu cha NAANDIKAJE KITABU? kimetoka. Kabla sijaweka kwa watu wengine zaidi, nakwambia wewe kwanza kwa sababu ni mtu muhimu kwangu.
Umuhimu wa kuandaa bajeti ya kutoa kitabu
Unaujua umuhimu wa kuandaa bajeti kwanza unapokuwa kwenye mchakato wa kutoa kitabu chako? Fikiria una rafiki yako ambaye amekuja kwako kuomba ushauri wa kuifanya bajeti yake ya kutoa kitabu itoshe, Je ungemshauri nini?.
Muda na wazazi – Kitabu kipya kutoka kwa Dr. Stanlaus
Ingizo jipya la kitabu kwenye shelfu za vitabu ni kitabu cha MUDA NA WAZAZI ambacho kimeandikwa na Dr. Stanlaus. Kitabu hiki ni moja ya projekti kubwa ambayo tumefanya kuanzia mwezi wa nane na tumeikamilisha mwezi huu wa tisa, tukihusika na kuhariri wake, kusanifu jalada na mpangilio wa ndani wa kitabu. Ni kazi bora sana ambayo tumeifanya.
Umuhimu wa kusoma vitabu
Kusoma vitabu limekuwa ni jambo gumu kwa wengi. Wengi wanashindwa, wachache wanajivuta vuta kusoma bila kumaliza vitabu walivyoanza kusoma na wachache kabisa wanaweza kusoma vitabu na kufaidika na maarifa yake.
Sababu saba (7) zinazofanya wasomaji wanunue au wasinunue vitabu.
Kila mwandishi wa vitabu hutaka sana kuona kitabu chake kinanunulika na kufikia wasomaji wengi wa vitabu. Kitabu kununulika au kutonunulika imekuwa ni kama kipimo cha mafanikio kwa mwandishi kujua kazi yake imepokelewaje na wasomaji. Lakini yako mambo mengi yanayochangia wasomaji kununua kitabu cha mwandishi fulani na si mwandishi fulani.
Programu sita (6) za DL Bookstore kukusaidia katika uandishi wa vitabu
Inatia moyo sana kuona idadi ya watu wanaotaka kuwa waandishi wa vitabu inaongezeka. Hii ni dalili nzuri sana kwa sababu inatoa picha ya mambo mawili; mosi, kuna mwamko wa watu kusoma vitabu, pili, watu wanataka kuacha alama ya mambo wanayofanya kwa vizazi vinavyofuata.
Vitabu vitano (5) vya biashara na uchumi muhimu kuvisoma
Mambo yamebadilika sana miaka ya hivi karibuni. Zamani kidogo, watu walikutana na changamoto ya kukosa maarifa muhimu kuhusu biashara na uchumi hasa walipotaka kuanza kufanya biashara au kutaka kujiongezea kipato zaidi. Lakini sasa, vitabu vya biashara na uchumi vimejaa tele kwa wewe kusoma na kufaidika na maarifa ya kukusaidia kufanya biashara bila ugumu wowote.
Unaisomaje kozi ya Siri 30 Za Kuwa Mwandishi Bora Wa Vitabu?
[Kutoka DaudiPages] Zikiwa zimesalia siku chache mno – Siku 5 tu, kozi itaanza tarehe 30.07.2022 – kozi ya Siri 30 Za Kuwa Mwandishi Bora Wa Vitabu kuanza, nimeona nigusie jambo hili; Unaisomaje kozi hii?. Nifanya hivi nikitambua kuwa kuna watu wengi, ikiwemo wewe, wanajiuliza hivi nitaisomaje kozi hii?. Natambua fika kabisa ratiba yako inaweza kuwa inabana, huna muda au una dharura na inakupa ukakasi kuamua uisome kozi au uiache.
Mambo tisa (9) niliyojifunza kwenye uzinduzi wa kitabu cha Jenga Wasifu Wako
Hivi majuzi nilihudhuria uzinduzi wa kitabu cha JENGA WASIFU WAKO kilichoandikwa na rafiki yangu Victor Lazaro (anayeonekana pichani). Uzinduzi huu ulifanyika pale New Safari Hoteli. Yako mengi nilijifunza na ninapenda kukushirikisha machache, kama mambo tisa (9) hivi.
Siri 30 za kuwa mwandishi bora wa vitabu
Siri 30 za kuwa mwandishi bora wa vitabu ni kozi maalumu iliyoandaliwa kiustadi na DaudiPages kukupa wewe maarifa na ujuzi muhimu kwenye uandishi wa vitabu. Baada ya kusoma kozi hii, utakuwa umejifunza mambo yafuatayo;