Naandikaje kitabu? sasa kimetoka!
Kitabu changu cha NAANDIKAJE KITABU? kimetoka. Kabla sijaweka kwa watu wengine zaidi, nakwambia wewe kwanza kwa sababu ni mtu muhimu kwangu.
Kitabu kinahusu nini?
Kitabu hiki ni toleo lililoboreshwa la kitabu cha Mbinu Rahisi Za Kuandika Kitabu. Wakati nilipotoa kitabu cha Mbinu Rahisi Za Kuandika Kitabu nililenga kuwasaidia watu wanaotaka kuingia kwenye uandishi wa vitabu lakini hawana watu wa kushika mkono ili kufanikisha ndoto zao.
Lengo bado ni lile lile isipokuwa nimeboresha zaidi na kufanya marekebisho fulani fulani baada ya kupokea maoni kutoka kwa wasomaji wengi waliosoma kitabu.
Katika toleo hilo jipya, nimeongeza vitu vingi ambavyo naamini, unapokisoma kitabu hiki utatoka ukiwa na nguvu mpya ya kuandika kitabu chako na hatimaye kutimiza ndoto yako ya kuwa mwandishi wa kitabu.
Naandikaje kitabu? Ni swali ambalo nimejibu katika kurasa zinazofuata. Mimi naamini, kuandika kitabu ni ujuzi ambao kila mtu anawez kujifunza
Kinapatiana wapi?
Kwanza nataka ujue kwamba, NIMEKUPA WEWE PEKE YAKO TU!, utakipata kwa Tsh. 3000 tu. Kinapatikana kwenye majukwaa yafuatayo,
Note: Ukienda DL Bookstore, tumia Visa ya Mpesa au Mastercard ya AirtelMoney kulipia. Kama utaenda Getvalue tumia namba yako ya kawaida ya mpesa, tigopesa, halopesa na kadhalika ili kulipia.
Zimebaki siku ngapi ofa hii niliyokupa iishe? Ofa itaisha baada ya siku 8.
Credit: DaudiPages
Karibu kwa maoni