Mtazamo sahihi uletao mafanikio - Kitabu kipya kutoka kwa Ruth Heslone
Ingizo jipya la kitabu kwenye shelfu za vitabu ni kitabu cha MTAZAMO SAHIHI ULETAO MAFANIKIO ambacho kimeandikwa na Mwl. Ruth Heslone. Kitabu hiki ni moja ya projekti kubwa ambayo tumeifanya ndani ya mwezi wa kumi (10), tukihusika na kuhariri wake, kusanifu jalada na mpangilio wa ndani wa kitabu. Ni kazi bora sana ambayo tumeifanya.
Mwandishi wa kitabu ametuandikia kionjo kifupi kukuonjesha na kukupa hamasa wewe kukiongeza kitabu hiki katika orodha yako ya vitabu vya kusoma mwezi huu wa 11. Je, anasemaje mwandishi?
Kumekuwa na mkanganyiko mkubwa katika jamii yetu leo kuhusu neno mafanikio huku wakiwepo watu wanaoamini katika kuwaza chanya mambo yote yatawezekana, wapo wengine ambao wanategemea wakiomba kila kitu kitajipeleka, na wengine wanaamini katika nguvu/akili zao na katika kupambana. Neno mafanikio limekuwa ni neno tata, na kila mtu amekuwa akilifafanua kivyake vyake.Lakini kitabu hiki kimejibu maswali mengi yaletayo mkanganyiko katika kanisa na jamii kwa ujumla. Kimelenga kila mtu ambaye moyo wake unatamani kufanikiwa katika njia iliyosahihi na ya kumpendeza Mungu na kuzungumzia kwa kina mtazamo sahihi utakaomsaidia mtu kufanikiwa katika mapenzi ya Mungu. Ni kitabu kitachobadilisha mtazamo wa mtu juu ya mafanikio na namna sahihi mtu anaweza kufanikiwa.
Ikiwa utahitaji kitabu wasiliana nasi kupitia namba 0787163013 au bonyeza hapa kuweka oda yako na tutakupigia. Angalia vitabu zaidi hapa na ufanye mwezi wa 11 kuwa bora sana kwako kwa kusoma vitabu vingi.