Jinsi ya kusoma kitabu ukiwa mtandaoni
Zamani kidogo ilikuwa huwezi kusoma kitabu kwa kutumia simu janja yako, tabuleti au kompyuta yako. Kusoma kitabu ingekutaka uwe na nakala ngumu, utulie mahali usome au uende maktaba iliyo jirani na wewe ili usome kitabu. Kama ungekuwa safarini, mfano kwenye daladala, ingekupasa utembee na nakala yako ili usome, sasa fikiria mtu aliyetaka kusoma vitabu vitano, si angebeba vyote atembee navyo? Shida gani hii!.
Lakini sasa, mapinduzi ya teknolojia kwenye vitabu yameboresha hali
hii na sasa kwa kutumia simu yako tu unasoma vitabu, tena vingi mno,
bila stress, raha iliyoje hii!. Lakini watu wengi bado wanashindwa
kuendana na mapinduzi ya teknolojia hii, wanalalamika kwamba
wanashindwa kusoma vitabu vilivyowekwa mtandaoni. Kumbuka kwamba, kwa
kusoma kitabu mtandaoni, namaanisha kwamba, usome kitabu kwa kutumia
simu, tabuleti na kadhalika.
Baada ya kusoma, mpaka mwisho, chapisho hili naamini hutapata changamoto tena ya kusoma kitabu chako ukiwa mtandaoni au online, kama wanavyosema vijana wa ki leo. Sasa unasomaje kitabu ukiwa mtandaoni?
Maduka ya mtandaoni ya vitabu.
Kwanza, ili usome kitabu mtandaoni itabidi uende kwenye duka la mtandao ambalo vitabu vinapatikana. Maduka ya mtandao yako mengi mno, ni wewe kujichagulia unalotaka kwenda. Duka zuri sana ambalo utapata kitabu unachotaka ni DL Bookstore, unajua unataka ujionee sasa hivi, hebu bofya hapa na utaenda moja kwa moja kwenye vitabu unavyotaka.
Kusoma kitabu unachokitaka.
Ukishaenda kwenye duka la mtandao (bonyeza hapa kwenda), kinachofuata ni kusoma kitabu kile ambacho umekipenda kukisoma. Utahitaji vitu viwili muhimu; namba yako ya simu (iwe ya tigo kwa sababu ya urahisi wa kulipia) na baruapepe tu. Unaanzaje sasa? Chagua kitabu kisha bonyeza READ NOW na baada ya hapo weka ile namba ya simu (ya tigo) na baruapepe yako.
Unakipataje kitabu?
Baada ya kubonyeza READ NOW na ukaweka namba ya simu na baruapepe, utabonyeza PAY NOW kulipia hicho kitabu na angalia kwenye simu yako muda huo huo, utaona ujumbe wa kuthibitisha hayo malipo na ukimaliza kuthibitisha, ingia kwenye baruapepe yako na utakuta risiti ya malipo ambayo ndani yake kitabu chako kimeambatanishwa.
Bonyeza kwenye link ya risiti ya kitabu, na mara unaponyeza tu, itafunguka kama inavyoonekana kwenye picha.
Sasa utabonyeza READ ONLINE ili kuanza kusoma kitabu chako. Lakini, kabla hujaanza kusoma itakulazimu ufungue akaunti ambayo ndiyo itakuwa maktaba yako ya mtandaoni, muda wowote ukiwa popote utaweza kuingia na kusoma kitabu chako bila stress. Hata ukipoteza simu au ukasahau simu mahali, utaweza kuingia kwenye akaunti yako kwa kutumia simu nyingine, muhimu kwako ni kukumbuka username na nenosiri tu.
Ukimaliza kufungua akaunti yako tu, tayari unakuwa umemaliza kazi. Kitabu kitafunguka na utaanza kusoma bila shida yoyote. Ukiwa kwenye akaunti yako, utaenda sehemu pameandikwa PURCHASES na vitabu vyote utavikuta hapo ambavyo utakuwa umevinunua kwenye duka la mtandao laDL Bookstore.
Sasa ukimaliza kusoma kitabu, usisahau kuki andikia REVIEW hicho kitabu ili na wengine ambao bado hawajakisoma, wakiona ile REVIEW yako basi nao watakinunua ili wakisome.
Karibu kwa maoni.